SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limempongeza Mkurugenzi wa MultiChoice Tanzania, Maharage Chande kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa MultiChoice Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Mei 20 mwaka huu, Kampuni ya MultiChoice Africa Limited, ilithibitisha uteuzi wa Wakurugenzi wawili, ambako Mtanzania Maharage Chande ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, anakuwa Mkurugenzi mpya wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Uteuzi huo uliotangazwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, unabainisha kuwa Maharage anachukua nafasi ya Stephen Isaboke aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki ambaye sasa anakuwa Mkuu wa Mamlaka (Group Executive Head of Regulatory). Uteuzi ambao unaanza Juni Mosi mwaka huu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, amesema uteuzi wa Maharage umezingatia uwezo na upeo wake mkubwa aliyouonyesha katika kipindi alipoiongoza MultiChoice Tanzania tangu alipojiunga nayo Juni 2016.

Rais wa RT, Anthony Mtaka, amesema familia ya Riadha Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi huo wa Maharage, hasa ukizingatia katika uongozi wake, MultiChoice Tanzania kupitia DStv, imekuwa mshirika mkubwa katika kuchangia maendeleo ya mchezo wa Riadha hapa nchini.

“Sisi kama Riadha Tanzania, tumepokea kwa faraja kubwa kupanda kwa cheo kwa Mtanzania mwenzetu Maharage Chande, hakika tutamkumbuka kwa mengi katika kusapoti maendeleo ya Riadha hapa nchini….Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya na bila shaka mapenzi yake katika mchezo wa Riadha atayaendeleza,” alisema Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera zake sana Maharage chande he deserves it!!! Big up ma Boy!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...