THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KATIKA UKUMBI WA MSEKWA MKOANI DODOMA

Na Lilian Lundo - MAELEZO,Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wanaafrika Mashariki kujiamini kuwa wanaweza kutekeleza miradi ya maendeleo bila kutegemea mataifa mengine.
Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa  akihutubia Bunge la Nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika mkoani humo kwa mara kwanza  tangu kuanza kwa Bunge hilo.
“Ninazungumza hili si kwamba hatuhitaji msaada au hatuhitaji ushirikiano, lakini ni lazima tuliweke hili wazi, kwamba tukiamua tunaweza na mifano ipo mingi ikiwemo Tanzania”. Alisisitiza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.
“Tanzania tunajenga reli ya kisasa yenye urefu wa kilometa 700.26 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa thamani ya shilingi Trilioni 7.6, tumeweza kununua ndege sita na pia tumejenga meli kubwa katika Ziwa Victoria bila kuomba mkopo popote,” amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameongeza kuwa wabunge wa Afrika Mashariki wanaowajibu wa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.
Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana na Jumuiya hiyo Rais Magufuli amesema kuwa kabla ya kuanza kwa umoja wa forodha mwaka 2005 biashara kati ya nchi wanachama ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.8 lakini baada ya kuanzishwa kwa umoja wa forodha imeongezeka hadi kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5.
Mbali na hayo Rais,  Magufuli ameshukuru uamuzi wa bunge hilo kufanyika mjini Dodoma ambapo kwa sasa Serikali imehamishia shughuli zake zote katika mkoa huo, na tayari watumishi wa serikali zaidi ya 3000 wameshahamia huku Rais Magufuli akitarajiwa kuhamia muda wowote mwaka huu.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Martin Ngoga amesema Bunge hilo linasubiri marekebisho ya mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ili  lugha ya Kiswahili ianze kutumika kama lugha rasmi katika vikao vya bunge hilo na katika jumuiya hiyo kwa kuzingatia azimio lililokwishapitishwa.
“Hatuoni sababu ya kutumia lugha za wageni wakati kuna lugha yetu ambayo tunazungumza ambayo ni kiswahili,” alisema Dkt. Ngoga.
Bunge la Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mkoani Dodoma katika ukumbi mdogo wa Bunge wa Pius Msekwa. Bunge hilo limefanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wa wimbo wa taifa uliokuwa ukipigwa ndani ya ukumbi wa Bunge wa  Msekwa ambapo alihutubia katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mkoni Dodoma.
 Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki (EALA).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika mkoni Dodoma.
  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuhutubia Bunge la EALA mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa tatu kutoka kulia, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga wa nne kutoka kulia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuwahutubia mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga mara baada ya kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki linalofanyika mkoani Dodoma. Picha na IKULU.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018. 
Mkutano huu umeitishwa baada ya mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC Mkutano huu umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018. 
Mkutano huu ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria, Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço , Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka; Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. 
Wengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho  Mhe. Edgar Lungu, Rais wa ZambiaRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati IIIMfalme wa Swaziland  Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço  Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),   Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda kumalizika mjini Luanda Angola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


JESHI LA MAGEREZA KUNOGESHA SHEREHE MAADHIMISHO YA MUUNGANO DODOMA


SPIKA NDUGAI ATEMBELEWA NA WAKURUGENZI WATENDAJI WA CLOUDS MEDIA GROUP, MULTICHOICE TANZANIA NA UJUMBE WA BUNGE LA MALAWI

 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na wageni wake Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Ndg. Joseph Kusaga (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji, Multichoice Tanzania Ndg. Maharage Chande (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza na mgeni wake Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Ndg. Joseph Kusaga (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Multichoice Tanzania Ndg. Maharage Chande
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji, Multichoice Tanzania Ndg. Maharage Chande (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Ndg. Joseph Kusaga 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutoka Bunge la Malawi Mhe. Kamlepo kalua (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, Ndg. Thomas Makiwa. PICHA NA OFISI YA BUNGE


WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI TFDA NA WATAALAMU WA DAWA KATIKA VIWANDA


MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

Msanii nyota wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours. 

Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola. 

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla. 

“Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond.

Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani Watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza. 

Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. 
“Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”
 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari.


TLS NI CHAMA CHA UMMA KIFANYE KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA - JAJI MKUU

Na Lydia Churi, Magreth Kinabo-Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) ni taasisi ya Umma na siyo binafsi hivyo amekitaka kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kisheria kwa kushirikiana na Mahakama na kuacha kujiingiza kwenye masuala ya uanaharakati na siasa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Jaji Mkuu amesema TLS ni chama huru cha kitaaluma kwa kuwa kilianzishwa kwa mujibu wa sheria kufanya kazi kwa manufaa mapana ya Umma.
“Hatuwezi kukubali chama hiki kikajisemea kuwa wao ni chama binafsi na tukakubali...Dhana ya ubinafsi haipo”, alisisitiza Jaji Mkuu.

Alisema jukumu la TLS ni Kuisaidia Serikali na Mahakama kuhusu mambo yoyote yanayogusa sheria, utawala wa sheria na kazi za kisheria na akaongeza kuwa dhana hii ndiyo inayoiunganisha Taasisi hiyo na Mahakama ya Tanzania.

Aidha, Jaji Mkuu amewataka viongozi wa TLS kushirikiana na Mahakama pamoja na Mihimili mingine ya dola  na kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari kwa kuwa hayawasaidii kuendeleza chama hiki muhimu kwa wanasheria nchini.
Jaji Mkuu pia amewashauri viongozi wa chama hicho kumuheshimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwa Sheria na Kanuni zote ni lazima zipitie kwake.
Alisema Mamlaka ya Baraza la Uongozi la TLS katika Kutekeleza Majukumu ya Umma ni kusaidia kuboresha elimu ya sheria na taaluma ya Sheria Tanzania na kuwawezesha wanataaluma wa sheria kupata elimu ya ziada ya sheria kwa kadri mabadiliko yanayotokea nchini na duniani.

Majukumu mengine ya TLS ni pamoja na kuwawakilisha, kuwatetea na kuwasaidia wanasheria Tanzania kuhusu mazingira ya kufanya kazi za kisheria na kuwasaidia wananchi wa Tanzania katika masuala ya kisheria yanayogusa Sheria.

TLS ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi kabla ya Uhuru na kukubalika kuendelea kuwepo kama Taasisi ya Kisheria kwa malengo ya kuanzishwa kwake kuelekezwa kwenye manufaa ya umma kwa kushirikiana na Mahakama, Bunge, pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chama hiki kilianzishwa kwa Sheria ya Baraza la Kutunga Sheria (Legislative Council) Namba 30 ya 1954 na ni moja ya Sheria nyingi za iliyokuwa Tanganyika kabla ya Uhuru, ambazo kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha Katiba ya Tanganyika  ziliruhusiwa kuendelea kutumika Tanganyika ilipopata Uhuru Disemba 9 mwaka 1961 kama Sheria za Tanganyika huru.


TPDC KUWANUFAISHA WANANCHI KWA GESI ASILIA MAJUMBANI

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi mradi wa uunganishaji wa gesi asilia kutoka katika bomba kubwa la gesi asilia linalomilikiwa na TPDC kwenda kwenye bomba dogo la usambazaji wa gesi asilia kutoka Ubungo hadi Mikocheni ambalo nalo linamilikiwa na TPDC ili kuongeza kiasi cha gesi asilia katika bomba hilo kwa lengo la kuwafikia watumiaji wengi zaidi. 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akikabidhi jukumu la ujenzi wa mradi wa uunganishwaji wa gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam katika eneo la Valvu namba 15 (Block Valve Station-BVS) ambapo ndipo bomba hilo litarajiwa kujengwa hadi eneo la Ubungo Maziwa litakapounganishwa na bomba dogo la usambazaji wa gesi asilia kuelekea Mikocheni Dar es Salaam. 

“Leo ni siku kubwa sana kwetu kama Kampuni ya Mafuta ya Taifa tunapokabidhi rasmi jukumu la ujenzi wa miundombinu ya kutoa gesi asilia kutoka kwenye bomba letu kubwa kwenda kwenye bomba letu dogo la usambazaji wa gesi asilia kazi ambayo itafanywa na kampuni ya SINOMA ambayo faida yake kubwa ni kulipa uwezo wa kubeba na kusambaza gesi nyingi zaidi itakayoruhusu uunganishwaji zaidi wa gesi asilia kwa watumiaji wapya katika maeneo yote ambayo bomba hilo linapita yaani Ubungo, Sinza, Chuo Kikuu, Survey, Mwenge na Mikocheni” alifafanua Kaimu Mkurugenzi. 

Akizungumzia wanufaika wa mradi huo pindi utakapokamilika, ndugu Musomba amesema kuwa, pamoja na kuendelea kusambaza kwa watumiaji wa zamani ambao ni MM I, MM II, MM III, TanPack na Iron and Steel wateja wapya watakaonufaika ambao tayari wameshakubaliana ni Coca Cola kwanza Limited na BIDCO na nyumba 70 katika awamu ya kwanza na kwamba wanatarajia kuunganisha kwa viwanda zaidi vitakavyokuwa tayari kwa muda wowote. 

Aidha akieleza kuhusu utaratibu wa uunganishwaji wa gesi asilia kwa watumiaji Mhandisi Musomba ameeleza kuwa, “Utaratibu ni wa kawaida sana kikubwa mteja tarajiwa anatakiwa kuwasilisha barua ya maombi ya gesi asilia kisha wataalam kufanya utafiti wa namna ya kumuunganishia mteja gesi hiyo na kwa upande wa watumiaji wa majumbani tunashauri pia nyumba kadhaa kuungana pamoja na kuleta barua kisha taratibu za kiutalamu za namna ya kuwafikishia gesi asilia zifanyike.” 

Kwa upande wake Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA, Lu Xiaoqiang ambao ndio Wakandarasi walioshinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo amesema kuwa, “Leo ni siku ya furaha kwa kuwa tumeweza kupata nafasi ya kutekeleza mradi wa TPDC wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka eneo la Ubungo bomba ambalo tunaamini litasaidia kukuza uchumi wa nchi nzuri ya Tanzania kwa kusambaza nishati viwandani na majumbani.” 
Akizungumzia gharama za matumizi ya gesi asilia majumbani Mhandisi Musomba amefafanua kuwa, “Matumizi ya gesi asilia ni ya gharama nafuu kulinganisha na mkaa na gesi za mitungi-LPG ambapo kwa mtumiaji wa gesi za mitungi mfano wa Kilo 15 ambayo itatumika kwa mwezi mmoja kama akitumia gesi asilia atatumia hadi miezi miwili na hivyo kuokoa karibu nusu ya gharama ya matumizi ya nishati majumbani lakini pia gesi asilia ni nyepesi kuliko hewa na hivyo kuwa salama zaidi kwa matumizi hata pale inapovuja kwa kuwa hupotea hewani.

” Jukumu la kusambaza gesi asilia ni la msingi kwa maeneo ya uchumi imara wa viwanda na hivyo TPDC inaendelea kufanya tafiti za kitaalamu za usambazaji wa gesi asilia katika maeneo mengine ya nchi yakiwemo Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga na Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba akieleza kwa kina Mradi Mpya wa Kuunganisha gesi asilia kutoka bomba kubwa hadi kwenye bomba dogo la Ubungo Mikocheni mradi ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi miwili. Piv
Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA, Lu Xiaoqiang akielza kwa waandishi wa habari namna watakaovyotekeleza ujenzi wa Miundombinu hiyo kwa ufanisi na wakati kadiri ya masharti ya mkataba. Pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Ubungo Tanesco, Sophia Fitina akielezea jinsi walivyoupokea mradi huo tokea umeingia katika eneo lao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (wa tatu toka kushoto) akiwa na  Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA ndugu Lu Xiaoqiang (anayemfuatia Kushoto) pamoja na wafanyakazi wanaotekeleza mradi huo. 


HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO APRILI 24, 2018


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 24.04.2018


Introducing "Awamu Ya Tano Uwanjani" By Ngoma Africa Band based in Germany


NIMERIDHISHWA NA MAADHALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

Waziri Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki  ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.
“Nimeridhika na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.”

Alhamisi Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama onesho lahalaiki, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr Florens Turuka, naMkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja  wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwapungia  wananchi, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA JENGO LA PSPF PLAZA NA TAWI LA BENKI YA NMB MJINI DODOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na viongozi mbalimbali baada ya kufunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa wafanyakazi wa umma la PSPF Plaza barabara ya Chimwaga mjini Dodoma leo April 23, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi mbalimbali akiakata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa wafanyakazi wa umma la PSPF Plaza barabara ya Chimwaga mjini  Dodoma leo April 23, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker kuashiria uzinduzi rasmi wa Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage mijini Dodoma leo April 23, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker pamoja na viongozi wengine kukata utepe  kuashiria uzinduzi rasmi wa Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kitengo cha huduma kwa wateja akiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Gavana Mkuu wa Benki ya Tanzania Dkt. Bernard Kibesse, Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Bi. Margareth Ikongo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kuzindua rasmi Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Gavana Mkuu wa Benki ya Tanzania Dkt. Bernard Kibesse, Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Bi. Margareth Ikongo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo  na viongozi wengine baada ya kuzindua rasmi Jengo la PSPF Plaza na Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018. Picha na IKULU


MKUTANO WA WADAU KATI YA SERIKALI, WAAJIRI PAMOJA NA SEKTA BINASFI KUHUSU MASUALA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KUFANYIKA MKOANI IRINGA, APRILI 30, 2018MAFUNDI MITAMBO REDIO 25 ZA KIJAMII WATEMBELEA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC KUJIFUNZA KWA VITENDO

MAFUNDI mitambo wa redio kutoka mikoa mbalimbali nchini wametembelea Shirika la Utangzaji Tanzania(TBC)kwa lengo la kupata mafunzo zaidi ili kuendelea kuboresha majukum yao kwa ufasaha.

Wakiwa TBC mafundi mitambo hao wamepata nafasi ya kutembelea vitengo mbalimbali ambavyo vinahusika na masuala ya utangazaji katika shirika hilo.

Mafundi mitambo hao wametembelea TBS jana jijini Dar es Salaam na hatua hiyo ni muendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), ambalo limeamua kuwapiga msasa mafundi mitambo kutoka redio 25 za kijamii Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa mujibu wa Unesco ni kwamba mafundi mitambo hao licha ya kuata mafunzo kwa kukaa darasani, watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kwenda kwao TBS ni sehemu ya kuendelea kuwajengea uwezo. Mafunzo ambayo ni sa siku saba yanatarajia kumalizika Aprili 25 mwaka huu.
Principle Engener kutoka TBC, Noel Mtenga akitoa ufafanuzi kuhusu gari la kurushia matangazo la TBC 1 linavyofanya kazi wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Mwahariri wa Habari za Kimataifa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Nyambona Masamba akiwaelezea mafundi mitambo wa Radio za jamii kuhusu namna wanavyopata habari za Kimataifa pamoja na jinsi wanavyozihariri kabla ya kurushwa hewani wakati wa ziara ya mafunzo yaliyofanyika katika Shirika la Utangazaji(TBC).
Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Ramadhan Mpenda akiwaelezea kiwaelezea mafundi mitambo wa Radio za jamii namna wanavyorusha habari kwenye moja ya studio ya TBC 1 iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Fundi mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Fanuel Elia akitoa ufafanuzi kuhusu namna wanavoweza kupangilia vipindi kwenye chumba cha kusimamia matangazo ya TBC 1 wakati wa ziara ya mafunzo kwa mafundi mitambo wa Radio za jamii.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agnes Kijo amesema ipo haja kwa wazalishaji wa dawa kuhakikisha wanazalisha dawa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vilivyoanishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kijo ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watalaam wa dawa katika viwanda  yaliyofanyika makao makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam , ambapo amefafanua nia ya mafunzo yanayotolewa ni kwa ajili ya kuzalisha dawa bora, vifaa tiba  na vitendanishi.

Amesema kuelekea uchumi wa viwanda ni pamoja na viwanda vitakavyojengwa ni lazima kufuata matakwa yaliyoanishwa na mamlaka za kudhibiti ubora huo ikiwemo TFDA.

Amesema uwezo wanawajengea ni kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni dawa, vifaa tiba pamoja na vitanishi kutokana na uzoefu wa WHO katika masuala ya ukaguzi wa viwanda .

Aidha amesema mafunzo hayo yakifanyiwa kazi itakuwa ni rahisi katika kufikia ubora ambao ndio unatakiwa kwa WHO katika kulinda afya ya mlaji.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na dawa(TFDA), Agnes  Kijo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuwajengea uwezo watalaam wa dawa katika viwanda na watendaji wa mamlaka hiyo yaliyofanyika Makao Makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.
 Mtaalam wa Mshauri  katika Uimarishaji wa wa Mamlaka za Udhibiti wa Dawa wa Shrika la Afya Duniani, Mohamed Refaat  akizungumza kuhusiana na mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa dawa katika viwanda ili kuweza kuzalisha dawa zenye ubora , mafunzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.
 Mtaalam wa Mshauri  katika Uimarishaji wa wa Mamlaka za Udhibiti wa Dawa wa Shrika la Afya Duniani, Mohamed Refaat   akitoa maelezo kwa watendaji wa TFDA na wataalam wa dawa katika viwanda  katika mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Makao Makuu ya TFDA jijiji Dar es Salaam.
Sehemu ya watendaji na wataalam wa dawa katika viwanda wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo na Shirika la WHO  yaliiyofanyika Makao Makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.


PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA MAFUNZO MAALUM YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imezindua kampeni maalumu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kueneza elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini. 

Kampeni hiyo inayokwenda sambamba na mashindano ya uchoraji michoro ya usalama barabarani imezinduliwa Dar es Salaam jana na ofisa wa Polisi, ASP Mbuya Matibu, kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usala,ma Barabarani.

AKizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, ASP Matibu,  alisema Puma Energy Tanzania, wana mchango mkubwa katika utoaji elimu ya usalama barabarani, hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.

Pia, aliwataka madereva nchini wasiendeshe magari kwa kukariri sheria,  bali wazitambue ili waweze kuzitumia vizuri kupunguza ajali.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema elimu ya usalama kwa wanafunzi ni muhimu, kwani inawapa uelewa wa matumizi ya barabara kwa usalama.

"Tunawaangalia sana watoto wa shule za msingi kwani wao wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani," alisema Corsaletti na kuongeza;


Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti akizungumza kuhusu wanavoshiriki na kufanikisha mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi hapa nchini ambapo kwa mwaka huu watatoa mafunzo kwa shule 22 kwa mkoa wa Ruvuma na Dar es Salaam.
Trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu akinzumgumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoa ya Dar es Salaam.
 Meneja Miradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend, Simon Kalolo akizungumzia mafunzo ya usalama barabarani wanayoyatoa kwa wanafunzi wa shule za msingi wakati wa uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo uliofanyika Makao makuu ya Kampuni ya Puma leo jijini Dar es Saaam.
 Mshindi wa mchoro 2017, mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Mbande, Nasri Mustafa akiwaonyesha  mchoro wake wa usalama barabarani alioshindawakati wa uzinduzi wa mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kutoka kulia, Meneja Miradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend, Simon Kalolo, meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu na Sajent Hussein Ramadhani. Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii

 Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, Trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo uliofanyika Makao makuu ya Kampuni ya Puma leo jijini Dar es Saaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA