Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji (hawapo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
Wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimiana na wazee wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...