Na Dotto Mwaibale, Ruvuma

WANANCHI wanaoishi katika Vijiji vya Mkenda na Mitomoni vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamesema changamoto kubwa waliyonayo ni mazingira magumu ya miundo mbinu ambayo inasababisha ugumu wa ufikishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

Wakazi hao wamesema kuwa, mazingira ya kufikisha dawa kwenye vijiji hivyo hutegemea zaidi usafiri wa kuvuka mto Ruvuma ambapo hulazimika kutumia boti,ambapo hata hivyo maisha yao yanakuwa na mashaka ndani ya mtumbwi hiyo ambayo iko wazi kutokana na mto huo kuwa na mamba wengi.

"Changamoto yetu kubwa ni usafishaji wa dawa kuja hapa kijijini kutokana na kutegemea zaidi mto huu ambao una mamba wengi, hata mwaka huu mwanzoni mtumbwi huu mnaouona ulipinduka na watu wakiwapo wauza mitumba waliuawa na mamba; lakini tunashukuru Bohari ya Dawa (MSD) kwani wao wanaweza kutuletea dawa kwa wakati" alisema Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa kijiji cha Mitomoni Omar Hassan.

Alisema ili kuondoa changamoto hiyo, wanaiomba serikali kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara, ili dawa hizo zisafirishwe kwa njia ya barabara badala ya kutegemea mto huo. Alisema yeye na kamati yake wamekuwa wakipokea dawa mara nne kwa mwaka kutoka MSD na kuzihakiki kwa ajili ya matumizi.

"Pamoja na changamoto ya miundombinu lakini tumekuwa tukihakikisha dawa zinazoletwa na MSD zinafika kituoni na kutumika ipasavyo,"alisema.Alisema kutoka Songea mjini hadi Kijiji cha Mitomoni, Songea vijijini, katika kituo hicho cha afya ni km 135 na MSD imekuwa ikihakikisha dawa hizo zinafika.
Wakazi wa vijiji vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na wafanyakazi wa Bobari ya Dawa (MSD), wakisaidia kushusha maboksi yenye dawa na kuyaingiza kwenye mtumbwi baada ya kupelekewa na MSD Kanda ya Iringa leo na baadae kuyapeleka katika Zahanati ya Kijiji cha Mitomoni.
Maboksi ya dawa yakiingizwa kwenye mtumbwi.
Wakazi wa Kijiji cha Mitomoni wakisubiri mtumbwi ili kuwavusha upande wa pili wa mto Ruvuma.
Dawa zikipelekwa Zahanati ya Mitomoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...