Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018. 

Mkutano huu umeitishwa baada ya mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC Mkutano huu umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018. 

Mkutano huu ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria, Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço , Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka; Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. 
Wengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho  Mhe. Edgar Lungu, Rais wa ZambiaRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati IIIMfalme wa Swaziland  Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço  Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),   Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda kumalizika mjini Luanda Angola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...