Said Mwishehe,Globu ya jamii 
 WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imetaja baadhi ya sababu zinazochangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa wanaume wengi nchini. 
 Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amesema utafiti wa kisayansi duniani unaonesha kuwapo kwa tatizo la nguvu za kiume. 
 Amefafanunua kwa Tanzania hakuna utafiti rasmi ambao umefanyika kubaini tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume nchini kwetu na kueleza ipo haja ya kufanya angalau utafiti ili kubaini udogo au ukubwa wa tatizo hilo. 
 Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ni ulaji wa vyakula vya mafuta, kutofanya mazoezi, matumizi ya ulevi wa pombe pamoja na uvutaji sigara. 
 "Hizo ni miongoni mwasababu ambazo kwa kiasi kikubwa zinaweza kusababisha mwanaume kuwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume.Hivyo tunashauri kwenye chakula ule chakula bora na si bora chakula,"amesema Dk.Ndugulile. 
 Ameeleza Serikali haijawekeza kwenye afya ya uzazi kwa wanaume bali imejikita zaidi kwenye afya ya uzazi kwa wanawake. 
 Ameweka wazi ukiangalia takwimu ya uzazi na akina mama kujifungua Tanzania haina shida lakini taarifa za kisayansi duniani zinaeleza kuna tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume duniani. 
 Dk.Ndugulile amesema kwenye aina ya dawa tano ambazo zimesajiliwa na Baraza la tiba asili na tiba mbadala kuna dawa inaitwa Ujana ambayo inahusika na mambo hayo ya upungufu wa nguvu za kiume. 
 Pia amesema tayari Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), nayo kuna dawa wanaendelea kuifanyia utafiti na watakapokamilisha itaingia kwenye matumizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...