Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza mpango kabambe wa kuviwezesha vikundi vya mazoezi ya kukimbia (Jogging club) kwa kuweka utaratibu wa mashindano  ya kila Mwisho wa Mwezi ambapo kikundi kitakachoshinda kitapatiwa kiasi cha shilingi Million 10 Kama mtaji wa kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kubaini idadi kubwa ya vijana hao wakimaliza mazoezi asubuhi hawana shughuli za kufanya hivyo wanakaa vijiweni na kitendo cha kukaa kijiweni wanaweza kushawishika kufanya vitendo vya uhalifu hivyo kwa kuwapatia mtaji itawawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali utakaowakwamua kiuchumi.
HUU NI MWENDELEZO WA RC MAKONDA KUWEZESHA AJIRA KWA VIJANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...