Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
KISHINDO kikubwa kimesikika katika maeneo ya barabara ya Chimala karibu na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam baada ya mti wa mbuyu uliopo ndani ya uzio wa hospitali hiyo unaodaiwa kuishi zaidi ya miaka 100 kuanguka.
Mbuyu huo umeanguka leo majira ya saa kumi alasiri na kusababisha kukatika kwa nishati ya umeme katika maeneo hayo ya hospitali ya Ocean Road, na pia umesababisha pia sehemu ya uzio wa hospitali hiyo kuvunjika.
Hata hivyo licha kuanguka na kufunga barabara ambayo imekuwa mara nyingi ikitumika kupitisha magari ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali, wakati huo hakukua na gari ya aina yoyote iliyokuwa inapita. Hivyo hakukuwa na madhara zaidi ya kubomolewa kwa uzio wa Hispitali ya Ocean Road.
Baadhi ya mashuhuda wakati mbuyu huo unaanguka wamedai kabla ya kuuanguka ulianza upepo mkali ulioutikisa.Pia inaelezwa dalili za kuanguka kwa Mbuyu huo ulianza tangu jana mchana baada ya kupiga radi wakati wa  mvua kubwa iliyonyesha. Baada ya radi hiyo waliabini mzizi wa Mbuyu huo kukatika na matokeo yake ukawa umeelemewa na hivyo ilipofika leo tisa Alasiri ndipo ukaanguka. 
Mafundi wa Umeme wa Tanesco wa kikosi cha dharura walifika na kuerekebisha mambo chap chap, na kuwezesha umeme kuendelea kuwaka baada ya kuuzima kwa muda.
Mashuhuda hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao wamedai walishtuka baada ya kusikia kishindo kikubwa wakati Mbuyu ukiwa  unaanguka na kusababisha mlipuko mkubwa wa umeme kutokana na  kukatika kwa nyaza za umeme zinazopita eneo hilo.
"Tunashukuru Mungu maana licha ya ukubwa wa mbuyu huu wakati unaanguka hakukuwa na mtu yoyote aliyekuwa anapita barabarani eneo hilo bali kuna gari moja ndogo ndiyo ilikuwa inapita lakini hata hivyo baada ya kupita eneo hilo ndipo mbuyu ukaanguka.
"Hivyo hakuna madhara yoyote ambayo yametokea zaidi ya kukatika umeme na sehemu ya uzio wa ukuta wa Ocean Road kubomoka,"amesema mmoja wa mashuhuda wakati anaielezea Michuzi Blogu ambayo waandishi wake walifika eneo la tukio kushuhudia kuanguka kwa mti huo unaodaiwa kuishi miaka zaidi ya 100.
 Mti wa Mbuyu wenye miaka zaidi ya 100 ukiwa umeanguka na kufunga barababra ya Chimala na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara pamoja na nishati ya Umeme leo  karibu na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi wakiangalia Mbuyu ulioanguka kufunga mawasiliano ya barabara inayotumiwa na viongozi wa wakuu wa serikalini ulioanguka leo jijini Dar es Salaam.

Mafundi wa Umeme wa Tanesco wakiwa katika eneo ulioanguka Mbuyu ambao ulifanya hitilafu ya nyaya za umeme leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...