Na. John Mapepele, Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa, Luhaga Mpina ametoa onyo kali kwa viongozi wa Serikali katika Halmashauri zote nchini wanayoihujumu operesheni maalum ya kitaifa ya kupiga chapa mifugo inayoendelea nchi nzima kwa kutoa taarifa za uongo zinazoonesha kuwa mifugo mingi imepigwa chapa tofauti na hali halisi ambapo amesema Wizara yake itapita kila Wilaya kufanya tathmini ya kina baada ya tarehe ya mwisho ya upigaji chapa kitaifa iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Marchi 31 mwaka huu ambapo watendaji watakaobainika kudanganya sheria zitachukua mkondo wake.

Aidha ametoa maelekezo kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kwamba mifugo yote inatakiwa iwe imepigwa chapa hadi tarehe ya mwisho iliyopangwa na kusiwe na visingizio vyaaina yoyote ikiwa ni utekelezazi wa Sheria ya Utambuzi,Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo Namba 12 ya Mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011. 

Maelekezo hayo aliyatoa jana akiwa Naibu Waziri wake Mhe. Abdalah Ulega na Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea mnada wa upili wa Kizota pembeni kidogo wa mji wa Dodoma kutoa tathmini ya zoezi la upigaji chapa nchini kabla ya siku ya mwisho ya upigaji chapa mifugo yote nchini ambayo ni tarehe 31/3/2018.

Waziri Mpina alisema, kulingana na takwimu ambazo Wizara imeletewa hadi tarehe 11 Machi, 2018 inaonyesha kwamba, jumla ya ng’ombe 16,744,355 kati ya 17,390,090 sawa na asilimia 96.3 ya ng’ombe wote nchini wamepigwa chapa. Aidha, jumla ya Punda 51,494 wamepigwa chapa nchini. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akimshika mkia ng’ombe kuangalia kama amepigwa chapa alipotembelea mnada wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma leo ambapo ametoa tathimini ya upigaji chapa unaoendelea nchini. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega(aliyenyosha mkono)akimwonyesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) chapa ya mifugo alipotembelea mnada wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma leo ambapo wametoa tathimini ya upigaji chapa unaoendelea nchini.Nyuma yake ni Kaimu Katibu Mkuu wa Mifugo Bi. Selina Lyimo, wakwanza kushoto mwenye shati la kitenge ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara Dkt. Angelo Mwilawa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo mkoani Kigoma hivi karibuni. Tarehe ya mwisho kitaifa ya uhitimishaji wa kupiga chapa mifugo yote nchini iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa ni 31/3/2018. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...