Na Bashir Yakub.
Inaweza kuwa nyaraka muhimu kama hati ya nyumba, mkataba wa mauziano au
mkataba mwingine wowote, wosia, kadi ya gari au ya mashine yoyote,hati ya
kusimamia mirathi, cheti cha ndoa au vyeti vinginevyo, na nyaraka nyingine
mbalimbali.
Nyaraka hii inaweza kuwa inatakiwa sehemu muhimu kama mahakamani ili
kuthibitisha shauri au kesi yako. Na inaweza ikawa ni nyaraka ambayo kuwepo
kwake ndio kushinda kwako na kutokuwepo kwake ndio kushindwa kwako.
Pamoja na umuhimu wa nyaraka hii bado umeitafuta kote pa kutafuta na
hukuweza kuipata. Au hukuitafuta madhali tu unajua ilishapotea au iko mikononi
mwa mtu ambaye hujui alipo na hawezi kupatikana. Katika mazingira ya namna
hiyo makala yataeleza vitu vichache vinavyoweza kusaidia kutoka Sura ya
sita,Sheria ya Ushahidi.
1. USHAHIDI WAKO.
Kitu kikubwa kinachomsaidia mtu kushinda kesi mahakamani ni ushahidi.
Kadhalika kushindwa kwako pia ni ushahidi. Ukisema hiki kiwanja au nyumba ni
yangu unatakiwa kuonesha hati au mkataba wa mauziano au vyote viwili.
Ukisema hili gari ni langu kadhalika uoneshe kadi yenye jina lako ama vinginevyo.
Ukisema nilikuwa na ndoa halali uoneshe cheti cha ndoa ama vinginevyo.
Ukisema nilimuuzia au kununua kitu fulani uoneshe mkataba ama risiti,vivyo
hivyo nk, nk.
Hakimu au Jaji si mtu ambaye anakuwa eneo la tukio na hivyo kuwa katika nafasi
ya kujua nini kilitokea huko. Yeye hajui chochote kilichotokea na hivyo taarifa zote
anazipata kwenu mnaoshitakiana. Kwa msingi huu yupo katika wakati mgumu
kuamua nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi kwa kitu ambacho hakushuhudia
na hakijui.
Kama hivi ndivyo kitu pekee cha kumuongoza hakimu/jaji huyu ambaye
hakuwepo wakati mnadhulumiana, ni ushahidi wa kila mmoja atakaowasilisha.
Hataangalia suraya mtu, kulia machozi kwa mtu, kuongea kwa kujiamini au kwa
unyonge kwa mtu, umri wa mtu, rangi ya mtu,wala jinsia, bali ushahidi ulio
uliowasilishwa na mtu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...