Ecobank
nchini Tanzania kuanzia mwaka huu inaanzisha mpango wa kutoa zawadi ya
ufadhili kwa wasichana wanaofanya vyema katika masomo yao kwenye shule
za serikali. Aidha pamoja na ufadhili huo ili kuwaweka katika hali ya
kuwa na uzoefu na kazi zao wanazosomea, watakuwa wanahakikisha wakati wa
likizo wanawafanyia mpango wa kujishughulisha na kazi hizo ili kuwa na
uzoefu.
Hayo
yamesema na Mkurugenzi Mkuu benki hiyo nchini Mwanahiba Mzee wakati wa
hafla ya mchapalo iliyofanyika hoteli ya Serena kusherehekea mafanikio
ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani mwishoni mwa wiki. Alisema
taasisi yake inaona umuhimu wa kumwezesha mtoto wa kike kusonga mbele
kama moto wa taasisi hiyo ya kifedha unavyosema ‘press for progress’
ikimaananisha kujikita katika kutafuta maendeleo.
Mkurugenzi
Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza kabla ya mgeni rasmi
ambapo alielezea kwa undani safari ya maisha kama mwanamke wakati hafla
mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake
duniani iliyoandaliwa na Ecobank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema
mwanamke anafanyakazi nyingi hivyo ni vyema kumwandaa tangu mapema ili
kujua majukumu yake kama mzalishaji mkuu kwenye familia.
Alisema
kwa sasa hawajaamua wanaanzia ngazi gani za ufadhili, lakini wanataka
kufanya kitu tofauti chenye kulenga kupromoti maendeleo ya mtoto wa kike
kama maazimio ya Beijing yanavyotaka kufikia asilimia hamsini kwa
hamsini katika ngazi za kiutendaji.
Alisema
sherehe hiyo ambayo inaambatana na siku ya mwanamke duniani
inasherehekewa katika nchi 33 zenye benki hiyo ikiwa ni sehemu ya
mkakati wa kibenki wa kuhakikisha kwamba wanawake wanasonga mbele kwa
kuwa idadi yao ni asilimia 49.55 ya watu waliopo duniani na wanahaki ya
kusaidia kukua kwa uchumi wa dunia, wa kaya na wakwao wenyewe kwa
kuwezeshwa.
Mshehereshaji
Babbie Kabae (kulia) akitambulisha wageni waalikwa kwenye hafla
mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake
duniani iliyoandaliwa na Ecobank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Anasema
pamoja na ukweli kuwa wanawake wameachwa nyuma kwa miaka mingi, taasisi
hiyo imejipanga kuhakikisha kwamba inakuwa na asilimia 50 kwa 50
ifikapo mwaka 2030 huku hapa nchini inakaribia asilimia 49.
Alisema
wakati sherehe hiyo ni kusherehekea mafanikio na kujifunza kutoka kwa
wanawake waliofanya vyema, wanawake wanatakiwa kujiuliza wamesaidiaje
wanawake wenzao kufikia ngazi ya juu kabisa ya uwezo walionao.
Alisema
katika taasisi yake wametengeneza mpango wenye vipengele vitano vya
kuhakikisha kwamba suala la jinsia linazingatiwa. Alitaja vipengele
hivyo kama kushawishi fikira za jinsia katika maeneo ya kazi kuona
kwamba kuna mizania. Kukabili fikira mgando dhidi ya wanawake, kuwezesha
mwanamke kuonekana wazi, kushawishi kuinua wanawake kwa kutwaa huduma
bora wanazozitoa na kusherehekea mafanikio ya mwanamke.
Mgeni
rasmi Mwanasiasa Mkongwe nchini na mpigania haki za wanawake, Mama
Getrude Mongella akitoa nasaha zake kwa wageni waalikwa na wafanyakazi
wa Ecobank Tanzania (hawapo pichani) wakati wa hafla mchapalo ya
kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani
iliyoandaliwa na Ecobank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema
amefurahishwa na jinsi wanawake majasiri kama Getrude Mongella
walivyoweza kupigania haki za wanawake wakikabiliana na makandokando
yake na kufanikisha maazimio ya Beijing ambayo yanatumika kumkomboa
mwanamke.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...