Mwandishi wetu ,Same
MKUU wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule amesema Makundi ya wanaweke kuanzia shule ya msingi, sekondari, vyuo, wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wanasiasa, viongozi katika nyanja zote wanatakiwa kukabiliana kuhakikisha Wilaya ya Same inawaandaa wanawake kushika  nafasi nyingi zaidi za juu katika uongozi na kuwa kati ya wanawake wanaomiliki biashara kubwa nchini. 

Sinyamule amewataka Wanawake hao kuwa na kauli moja tu ya kuwa kumiliki viwanda ni haki yao.

na kuwataka kuanza kutafuta maeneo ya uwekezaji na kufikiria kukua zaidi, kuchukua hatua bila kusubiri, kushikana mkono.

"Serikali ya Wilaya imejipanga kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali kuu
yaanza kuanza kuunda mabaraza ya kata, hili yaweze kutenga maeneo ya uwekezaji vijijini na kuainisha maeneo ya wanawake, yaahidi kutoa % ya wanawake,  vijana na walemavu kwa ukamilifu. pamoja na kuanzisha soko la barabarani kukuza bidhaa za wanawake" Amesema 

Amesema wilaya  yake kwa kushirikisha wadau kujenga majengo ya kuwezesha viwanda vya wanawake na kutetea haki ya elimu kwa watoto wa kike. 

Pia amesema mimba kwa wanafunzi zinaonyesha dalili ya kupungua  kwa kipindi cha mwaka 2018 hivyo kuwatka wakzi wa Same kuwatia nguvuni wanaowapa mimba wanafunzi ili nao wapate fundisho na kuvitaka  vyombo vya ulinzi kuendelea kuwasaka wote. 

Hivyo kuwataka  wanawake Same kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Wilaya kwani wengi ni wanawake, wakiweza ni ushindi kwa wanawake wote. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Wilaya ya Same yaliyokuwa na lengo la kupinga ukatili kwa Wanawake.
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sinyamule akikagua Bidhaa za Wajasiliamali waliohudhuria katika Maonyesho ya Siku ya Wanawake Duniani.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria Kongamano la Wanawake lililokuwa likifanyika katika Wilaya hiyo katika maadhisho ya siku ya Wanawake Duniani
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sinyamule , akiwa katika picha ya Pamoja na uongozi wa Wanawake Wilaya ya Same.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...