Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumter Mshama

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MKUU wa wilaya ya Kibaha Assumter Mshama ametoa ahadi ya fedha kiasi cha sh. 100,000 kwa mtu atakayetoa taarifa na kuwafichua wafanyabiashara wanaoendelea kuuza pombe aina ya viroba ambazo zilizopigwa marufuku na serikali .

Aidha amesema ,hata wafumbia macho wafanyabiashara wa maduka yanayouza vileo ambao hawana leseni ,kwani watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufungiwa biashara zao. Aliyasema hayo mjini Kibaha alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye baadhi ya maduka yanayouza vileo na baa ambazo wamiliki wake wanatuhumiwa kuuza viroba.

Mshama alisema  wafanyabiashara hao wa vileo wanakiuka agizo la serikali hivyo kwa atakayebainika kuuza pombe hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria. “Leo tumekamata viroba viwili hii inaashiria kuwa pombe hizi zipo,”

"Ninatangaza donge hilo nono ili kuleta hamasa ya ukamataji wa wauzaji wa pombe hizo ambazo ziliwaharibu hasa vijana na watu ambao walikuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na kuelemewa na ulevi," alieleza Mshama.
Mshama alieleza kwamba, kutokana na serikali kuzuia pombe hizo hali imeanza kuwa nzuri kwani vijana angalau wameachana na unywaji wa pombe hiyo na kupunguza vitendo vya kihalifu.

“Sasa tunatembea bila wasiwasi wa kuibiwa lakini kipindi cha nyuma akinamama walikuwa wakiporwa mikoba yao ama simu zao ,;"na madereva bodaboda nao wamebadilika hata ajali za bodaboda zimepungua,” alisema Mshama. Alitoa maelekezo kuwa wamiliki wa biashara za vileo /baa hawapaswi kufungua biashara muda wa kazi .

Mshama alisema, suala hilo linapaswa lisimamiwe na watendaji wa mitaa na vijiji kwa kuwa tayari walishapewa maelekezo. Nae mkazi wa eneo la Maili Moja, Ally Ramadhan alisema ,ili kufanikisha ukamataji wa viroba serikali inapaswa kushirikiana na wananchi kwa ajili ya kupata taarifa za wauzaji wa pombe hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...